 |
|
Previous Blogging
|
|
New Page 1
|
|
View our Pages |
-Musa Hussein -Music Mayday -Peace Clubs
wish to have your Own Page at bonge
Kurasa, write to
blog@bongekurasa.com |
|
|
|
|
added on 2012-05-19 18:52:48 by Admin
Chelsea ya England imeshinda Kombe la Klabu Bingwa Ulaya
2012 baada ya kuwashinda Bayern Munich ya Ujerumani kwa mikwaju ya penati 4-3.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1 baada ya dakika 90 za kawaida na
kulazimika kwenda katika dakika za nyongeza. Hata hivyo timu hizo ziliendelea
kuwa sare na hivyo kulazimika kuamiliwa kwa mikwaju ya penati.
Awali, Thomas Muller alindika bao la kwanza kwa Bayern Munich katika dakika
ya 83, lakini Didier Drogba alisawazisha kwa mpira wa kichwa katika dakika ya
88.
Mchezo uliendelea katika muda wa ziada na dakika nne za kipindi cha kwanza
Drogba alimfanyia faulo Frank Ribery ndani ya eneo la hatari na kusababisha
penati. Arjen Robben alipiga penati hiyo lakini ilidakwa na kipa Petr Cech.
|
added on 2012-05-19 18:16:14 by Admin
Global Network of Religions for Children- FOURTH FORUM
Young Artists to End Child Poverty
THEME:ENDING POVERTY, ENRICHING CHILDREN; INSPIRE. ACT. CHANGE
Tell your Community how to end poor Governance & Corruption
Show your World how to end War and Violence.
Inspire your Friends how to end Unequal Distribution of Resources.
more info: Please visit our bunner
|
added on 2012-05-17 12:02:44 by Admin
|
|
|
Quality Centre Mall - Dar es Salaam |
Quality Centre is all set to make a difference in shopping, relaxation and enjoyment for Tanzania. It is the largest shopping centre in the country and was built to meet international standards. Quality Centre offers mixed-use retail outlets, super markets, restaurants, family entertainment centres, banks, and movie theaters.
Shopping Hours
Weekdays 10 am – 8 pm
Weekends/Holidays 10 am – 9 pm
Please note that opening hours for Savannah Lounge, Uchumi and Cineplex are different.
Contact:
Quality Centre Mall
Nyerere Road, Plot no. 25
P.O. Box 40563, Dar es Salaam
Tanzania
Website: http://www.qualitycentremall.com/
 Shopping at Quality Centre Mall-Dar es Salaam
|
added on 2012-05-17 09:51:27 by Admin
Hayo yamebainika baada ya Mamlaka ya Kampuni ya CORDIAL Transport Services P.L.C ya usafiri wa daladala Dar es Salaam kutoa mapendekezo hayo ya viwango vya nauli mpya za usafiri.
Kupitia mapendekezo hayo yamependekeza kwa usafiri wa njia fupi jijini Dar es Salaam kupata hadi Sh. 450 kutoka Sh.300 ya awali.
Na kwa njia ndefu watalazimika kulipa nauli ya sh 600 kutoka 400 ya sasa na wale wanaotoka umbali mrefu zaidi watalipa 700 kutoka 500 .
Maombi hayo yamewakilishwa kwa madai ya ongezeko la gharama za uendeshaji wa usafiri.
Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano wa Sumatra, David Mziray amesema, kutokana na mapendekezo hayo imeandaa mkutano wa kukusanya maoni utakaowajumuisha wadau wa sekta ya usafirishaji
|
added on 2012-05-16 02:35:29 by Admin
MAWAKILI wanaomtetea mwigizaji wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji, wamewasilisha Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam maombi ya uchunguzi wa umri wa mteja wao.
Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidaiwa kutenda kosa hilo nyumbani kwa marehemu Machi 7, mwaka huu.
Mawakili hao waliwasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 7, mwaka huu wakiiomba iamuru kesi ya msanii huyo isikilizwe katika mahakama za watoto wakidai kuwa mteja wao ni mtoto.
Hata hivyo, mawakili hao waligonga mwamba baada ya mahakama hiyo kutupilia mbali ombi hilo ikisema ingawa kesi bado iko katika hatua za awali, haiwezi kufanya uchunguzi huo kwa kuwa haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.
Jana, mawakili wanaomtetea msanii huyo waliwasilisha maombi Mahakama Kuu wakiiomba itoe uamuzi kama Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kuamua ufanyike uchunguzi wa umri halali wa msanii huyo kwa kuwa wanaamini kuwa ina mamlaka hayo.
Katika maombi hayo namba 46 ya mwaka 2012, yaliyosilishwa na Wakili Peter Kibatala kwa niaba ya jopo la mawakili hao, pia wanaiomba Mahakama Kuu kama itaridhika kuwa Mahakama ya Kisutu haina uwezo huo, basi yenyewe ifanye uchunguzi huo.
Akifafanua juu ya maombi hayo, Kibatala ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alisema Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, Kifungu cha 113 inaruhusu Mahakama kufanya uchunguzi wa umri wa mshtakiwa.
Wakili Kibatala alisema lengo la uchunguzi huo ni kuifanya ijiridhishe kama mshtakiwa ni mtoto au ni mtu mzima kwa lengo la kuangalia maslahi ya mtoto.
“Baada ya uchunguzi huo, mahakama ikijiridhisha kuwa ni mtoto, basi mwenendo wa kesi hiyo utaendeshwa kwa maslahi ya mtoto kwa mujibu wa Kifungu cha 4(2) cha Sheria ya Mtoto,” alisema.
Alisema kifungu hicho huelezea ulinzi na maslahi ya mtoto katika uendeshaji wa kesi kwa watoto wanaokinzana na sheria.
Mawakili hao wakiwa katika Mahakama ya Kisutu, walidai kwamba msanii huyo ana umri wa miaka 17 na kwa maana hiyo bado ni mtoto na kesi yake haipaswi kusikilizwa katika mahakama za kawaida kama mtu mzima.
Katika uamuzi wake, Hakimu Mkazi Augustina Mmbando anayesikiliza kesi hiyo alisema bado iko kwenye upelelezi na kwamba kulingana na jinsi ilivyo isingekuwa busara kuamua hoja yoyote na aliutaka upande wa utetezi uwasilishe maombi hayo kupitia Mahakama Kuu.
Wakati akiwasilisha maombi hayo awali Mahakama ya Kisutu, kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea msanii huyo, Wakili Kennedy Fungamtama alidai kuwa mteja wao ana umri wa miaka 17 na si 18 kama inavyotamkwa mahakamani.
Alidai kuwa hata cheti cha kuzaliwa walichokiwasilisha mahakamani, kinaonyesha mahali na tarehe aliyozaliwa mshtakiwa hivyo kuwa na umri wa miaka 17.
Fungamtama alidai kuwa kulingana na Sheria ya Mtoto ya 2009, inatafsiri kuwa mtoto ni yule aliye na umri chini ya miaka 18 hivyo katika suala la mteja wao, alipaswa kushtakiwa katika mahakama ya watoto.
Hata hivyo, upande wa mashitaka kupitia kwa Wakili Elizabeth Kaganda ulipinga maombi hayo na kudai kuwa bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo na hivyo kuomba wapewe muda zaidi.
Wakili Kaganda pia alidai kuwa hata jina linaloonekana katika cheti cha kuzaliwa cha mshtakiwa huyo linasomeka kama Diana Elizabeth wakati mshtakiwa huyo ametajwa mahakamani hapo kama Elizabeth Michael.
Akijibu hoja hiyo, Wakili Fungamtama alikiri jina hilo kusomeka Diana Elizabeth na kusema kuwa ni jambo la kawaida hasa kwa Wakristo kuwa na majina mawili.
Mbali na Kibatala na Fungamtama, mawakili wengine katika jopo hilo ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Joaquine De- Melo.
Jopo la mawakili hao wanaomtetea msanii huyo linahitimishwa na Fulgence Massawe kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Mei 21 mwaka huu na msanii huyo bado anaendelea kusota rumande kutokana na kesi inayomkabili kutokuwa na dhamana.
|
added on 2012-05-16 02:29:55 by Admin
|
|
|
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba |
ASEMA NAPE ANAIGEUZA CCM MALI YAKE,PINDA YUKO MBALI NA WANANCHI, KINGUNGE PIA ACHARUKA
BAADA ya ukimya wa muda mrefu, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba ameibuka katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho (Nec) na kumtuhumu Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kwamba amekigeuza chama kuwa mali yake binafsi.
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, zimesema kwamba Makamba alisema hatua ya Nape kugeuza chama hicho kama taasisi yake binafsi ndiyo ambayo imesababisha kikose mwelekeo.
Makamba licha ya kuelekeza mashambulizi yake kwa Nape, alimrushia pia kombora Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwa ana uhusiano mdogo na wananchi.
“Mzee (Makamba) amesema hivi sasa CCM imekuwa kama jogoo anayepelekwa kwa mganga, kila anakoelekezwa ndo huko, hali hiyo ndiyo inakikumba CCM hivi sasa. Amemweleza Nape kuwa amegeuza chama kama mali yake binafsi, anafanya mambo nje ya utaratibu na anaangaliwa tu.”
Makamba alidai kuwa badala ya sekretarieti kushughulikia matatizo ya chama, imekuwa ikihangaika na watu kwa sababu ya kutofautiana nao misimamo na wakati huo wakijidai kuzika tofauti ili kukiimarisha.
Nape alipoulizwa kuhusu suala hilo alipuuza na kusema: “Si kweli, lakini ninyi andikeni tu maana tumewazoea.”
Alipotakiwa kueleza kama Kingunge na Makamba walisema nini dhidi yake katika kikao cha Nec alijibu: “Walikuwapo, lakini hakuna kati yao aliyenitaja hata kwa jina.”
Nape alitumia muda mwingi kulalamika kuwa taarifa nyingi ambazo zimekuwa zikitolewa kutoka ndani ya mkutano huo uliomalizika jana zimetoka kwa watu aliowataja kuwa wana maslahi nazo binafsi na kuhoji,” Kwa nini msiwe mnasubiri taarifa rasmi (za chama) ili habari iwe ya ukweli zaidi?”
Mkongwe mwingine wa chama hicho, Kingunge Ngombale-Mwiru, ambaye anadaiwa kusikitishwa na vitendo vya rushwa na ugomvi vinavyoendelea ndani ya chama huku vikiangaliwa na viongozi kama vile vinakistawisha wakati vinakiporomosha.
Kingunge alidai kuwa hivi sasa chama hicho kimetawaliwa na matajiri ambao ndiyo wanaopata nafasi za uongozi na maskini wanawekwa kando.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja aliunga mkono suala la Pinda kuwa na uhusiano mdogo na wananchi na kwamba, amekuwa mkimya zaidi na hamsaidii Rais Jakaya Kikwete.
“Yule Mwenyekiti wa Shinyanga, amemweleza Pinda kuwa ng’ombe wakila mazao mtu wa kwanza kuchapwa viboko ni mchungaji, halafu mmiliki anatozwa faini baadaye. Hivyo, alitakiwa kuwajibika kwanza kabla ya mawaziri walioondolewa,” kilidokeza chanzo chetu.
Mgeja alidai kuwa uwajibishwaji wa mawaziri, haukuzingatia haki kwa sababu George Mkuchika, Profesa Jumanne Maghembe na Hawa Ghasia walilalamikiwa, lakini kilichofanywa ni kutoa kafara wengine na hao kubadilishiwa wizara.
Pia, inadaiwa kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwataka wajumbe kuzika tofauti zao ili kuweka msimamo wa pamoja kwa ajili ya ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa 2015 na kwamba adui namba moja wa CCM hivi sasa ni Chadema.
Rushwa yakishtua chama
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema Nec imejadili changamoto zinazokikabili chama kwenye uchaguzi unaoendelea na kubaini kuwa rushwa imekithiri.
Nape alisema tishio la rushwa ni kubwa na mgombea atayakayethibitika kujihusisha na vitendo hivyo rushwa ataondolewa mara moja, huku viongozi na watendaji wakitahadharishwa kuchukuliwa hatua za nidhamu.
“Kwa kisingizio cha kuwasalimia wajumbe, kuwapa nauli au kujitambulisha. Mgombea atakayethibitika anazunguka au amezunguka ataondolewa bila kuchelewa katika orodha ya wagombea,” alisema na kuongeza:
“Kwa watendaji na viongozi wa chama ngazi zote kuanzia sasa ni marufuku kuwatembeza ndani ya maeneo yao, kwa nia ya kuwatambulisha kwa wapiga kura. Mtendaji au kiongozi atakayebainika anakiuka agizo hili, atachukuliwa hatua za nidhamu mara moja.”
Pia, Nape alisema kuanzia sasa ni marufuku kwa watendaji na viongozi wa chama ngazi zote kuwaitia wagombea, wajumbe wa mikutano ya uchaguzi kwa lengo lolote, kwani vikao vya aina hiyo havimo katika katiba.
Alisema vikao vya aina hiyo ni haramu na vinapalilia rushwa na kuongeza kwamba wanachama wa CCM wanatakiwa kupiga vita rushwa na kutoa taarifa ya vitendo hivyo katika ofisi za chama na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Aliitaka Takukuru kutomuonea aibu au kumuogopa mtu anayejihusisha na vitendo vya rushwa badala yake wamchukulie hatua.
Mishahara na chakula
Kuhusu mishahara ya watumishi wa umma na mfumuko wa bei ya chakula, Nape alisema Nec imeagiza Serikali kuhimiza waajiri kupandisha mishahara na malipo mengine kwa wafanyakazi wao ili waweze kumudu gharama za maisha.
Alisema gharama za maisha zimepanda na mishahara inayolipwa haiendani na hali halisi. Alisema nayo Serikali inatakiwa nayo kupandisha mishahara kwa watumishi wake.
“Serikali idhibiti malipo ya huduma ya ndani kwa kutumia fedha za kigeni, hasa Dola ya Marekani. Pia, iongeze udhibiti wa maduka na hoteli zinazofanya biashara ya fedha za kigeni ili kuondoa hujuma kwa uchumi wa nchi inayofanywa kutokana na uhuru uliokithiri katika biashara hii,” alisema.
Nape alisema Serikali inatakiwa kuweka jitihada zaidi za kudhibiti ulanguzi wa bidhaa muhimu na upandishaji holela wa bei za vyakula, kodi za nyumba na usafiri.
Alisema Nec imeagiza Serikali kuendelea kuchukua hatua za muda mrefu na kati za kukabiliana na tatizo la mfumuko wa bei.
“CCM inaiagiza Serikali kuchukua hatua za haraka na muda mfupi ikiwamo kuangalia upya baadhi ya kodi katika vyakula pamoja na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika sukari,” alisema Nape.
Pia, Nape alisema wameagiza Serikali kupitia upya utaratibu wa ruzuku ya mbegu na mbolea ili upanuliwe kunufaisha wakulima wengi.
Alisema Nec imeitaka Serikali iongeze kasi ya utekelezaji wa mpango wake wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula nchini, hasa kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Nafaka ya Taifa (NFRA), ikiwamo kujenga maghala zaidi ya mazao ya chakula maeneo ya uzalishaji na kutenga fedha nyingi zaidi kwa ununuzi wa mazao hayo.
“Wakati wa uhaba wa vyakula maeneo ya mijini, kasi ya kupeleka chakula maeneo hayo iongezwe na utaratibu mzuri zaidi wa usambazaji chakula utumike ili walaji na siyo wasafirishaji na wasindikaji, wanufaike,” alisema.
SOURCE: Mwananchi |
added on 2012-05-16 02:14:44 by Admin
|
|
|
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa,Dickson Maimu akizungumza na waandishi wa haba |
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), imebaini kuwa Jeshi la Polisi lina askari 700 wenye majina yanayofanana na waajiriwa wengine serikalini huku Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likiwa na askari 248.
Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Dickson Maimu alisema jana Dar es Salaam kwamba watumishi hao wamebainika kutumia cheti kimoja cha elimu na mtu mwingine jambo ambalo lilikuwa changamoto kubwa wakati ilipoanza uandikishaji kwa watumishi wa Serikali.
Maimu alikuwa akitoa kwa waandishi wa habari, taarifa ya utekelezaji wa mradi wa vitambulisho vya Taifa na kubainisha kuwa hiyo ni dalili kwamba watumishi wake watakabiliwa na changamoto kubwa katika kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anapata kitambulisho cha uhakika.
“Kwa hivi sasa maeneo tuliyopitia tumegundua kuna utumiwaji wa vyeti mara mbili vyenye jina moja na mkitaka niwatajie. JWTZ tumekuta watu 248 na Polisi watu 700 ambao vyeti vyao vinatumiwa na watu wawili tofauti,” alisema Maimu.
Kuhusu hali ya mradi, Maimu alisema wameamua kisitisha kwa muda uzinduzi wa vitambulisho hadi Juni Mosi, mwaka huu siku ambayo vitambulisho hivyo vitaanza kutolewa kwa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam.
“Mamlaka ya vitambulisho vya taifa imekamilisha hatua zote na tuko tayari kuzindua mradi wetu na kutoa vitambulisho. Hata hivyo, zimejitokeza changamoto na mahitaji ya msingi kutoka kwa wadau wetu muhimu ambavyo hatuna budi kuvifanyia kazi kwanza ili kitambulisho kiwe kimekidhi mahitaji yote,” alisema.
Maimu alisema mahitaji makubwa yaliyojitokeza ni mfumo wa vitambulisho kutambua na kuingiza anuani za makazi na postikodi, kufanya usajili wa pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na kuwezesha rasimu ya ukusanyaji maoni ya Katiba Mpya chini ya tume iliyoundwa.
Maimu alisema taarifa hizo zitasaidia kupatikana kwa urahisi taarifa kamili za wakazi katika eneo husika, chini ya Serikali za Mitaa.
“Tayari tumeshafanya mazungumzo na mkandarasi (Iris) kuweza kuingiza katika mfumo mahitaji haya makubwa ya wadau wetu,” alisema Maimu.
Alisema maandalizi ya awamu ya kwanza yamekamilika na Nida iko tayari kutoa vitambulisho kwa awamu ya kwanza, baada ya mkandarasi kukamilisha kuingiza mabadiliko makubwa mawili ya mfumo wa daftari la kielektroniki.
“Mabadiliko hayo ni anwani za makazi na simbo za posta(postal code), pia kufanya usajili wa pamoja na Nec,” alisema Maimu.
Alisema Serikali imeamua kuwa uandikishwaji wa vitambulisho unapaswa uende sambamba na ule wa wapiga kura ili kupunguza gharama na usumbufu unaoweza kujitokeza kwa kuwaita watu walewale kujiandikisha mara nyingi ndani ya kipindi kifupi.
“Baada ya kutambua umuhimu wa kupunguza gharama za uendeshaji pamoja na kupunguza adha kwa wananchi, Nida imefanya majadiliano na Nec na kukubaliana kuwa zoezi la usajili lifanyike kwa kushirikiana kwa pamoja katika nyanja za vifaa, watumishi na wakandarasi,” alisema Maimu.
Alisema kutokana na hali ilivyo, kazi hiyo itafanyika kwa mwaka mmoja na nusu badala ya miaka minne kama ratiba ya awali ilivyokuwa ikionyesha.
“Imekuwa lazima sasa kutumia vitambulisho kwa ajili ya uchaguzi na Katiba Mpya ambayo ‘referendum’ (kura za maoni ) itakuwa mwaka 2014,” alisema na kuongeza kuwa Maimu alisema mchakato wa usajili utatanguliwa na ujazaji wa madaftari ya wakazi.
“Madaftari haya ni muhimu katika kutunza kumbukumbu za wananchi wanaoishi katika eneo husika na pia kusaidia upatikanaji wa haraka wa taarifa za wananchi pindi zinapohitajika.”
SOURCE: MWANANCHI - May 14 |
added on 2012-05-16 01:55:07 by Admin
|
|
|
Tanzania Football Federation (TFF) |
ASPIRE KUANZA KUSAKA VIPAJI MEI 21
Mchakato wa kusaka vipaji kwa chipukizi wenye umri chini ya miaka 14 kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream ambao uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utafanyika kuanzia Mei 21 mwaka huu.
Vituo vitakavyohusika ambavyo kila kimoja kinatakiwa kuwa na watoto wasiopungua 176 na tarahe ya kufanyika mchakato huo kwenye mabano chini mng’amua vipaji (scout) kutoka Hispania ni Morogoro (Mei 21 mwaka huu saa 3 asubuhi) na Bagamoyo mkoani Pwani (Mei 21 mwaka huu saa 8 mchana).
Vingine ni Kawe, Dar es Salaam (Mei 22 mwaka huu saa 3 asubuhi), Makongo, Dar es Salaam (Mei 22 mwaka huu saa 8 mchana) na Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam (Mei 26 mwaka huu saa 9 mchana).
Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16 duniani kwa Tanzania una jumla ya vituo 14. Vituo vingine ni Kigamboni, Tandika, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni na Tabata.
Watoto watakaochaguliwa katika mchakato huo watakwenda katika mchakato mwingine kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Nairobi, Kenya.
Watakaofuzu kutoka hapo ndiyo watakaokwenda kwenye vituo vya kuendeleza vipaji (centre of excellence) vya Aspire Football Dreams. Aspire ina vituo viwili vya kuendeleza vipaji ambavyo viko Doha, Qatar na Dakar, Senegal.
TWIGA STARS KUJIPIMA KWA BANYANA BANYANA
Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) inatarajia kucheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Afrika Kusini (Banyana Banyana) itakayofanyika Mei 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Twiga Stars inayojiandaa kwa mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia imeingia tena kambini jana (Mei 14 mwaka huu) kujiwinda kwa mechi hiyo itakayochezwa Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa.
Banyana Banyana pia iko katika kinyang’anyiro cha kutafuta tiketi ya Fainali za Nane za AWC ambapo katika raundi hii ya pili imepangiwa Zambia na itaanzia mechi hiyo ugenini jijini Lusaka.
Mei 12 mwaka huu Twiga Stars ilicheza mechi ya kimataifa ya kujipima nguvu dhidi ya Zimbabwe (Mighty Warriors) iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kambi ya timu iko Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Ruvu mkoani Pwani.
Naye Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Charles Boniface Mkwasa katika kuimarisha kikosi chake kabla ya mechi ya Jumapili dhidi ya Banyana Banyana amemwita tena kikosi mshambuliaji mkongwe Esther Chabruma.
Wakati huo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Rwanda kuchezesha mechi hiyo ya AWC kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Ethiopia.
Waamuzi hao ni Angelique Tuyishime atakayepuliza filimbi wakati waamuzi wasaidizi ni Sandrine Murangwa, Speciose Nyinawabari na Salma Mukansanga. Kamishna wa mchezo huo wa kwanza ni Catherine Adipo kutoka Uganda.
Mechi ya marudiano itachezwa Dar es Salaam wiki mbili baadaye ambapo mshindi atapata tiketi ya kucheza Fainali za Nane za AWC zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
WATUNISIA KUICHEZESHA STARS ABIDJAN
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeteua waamuzi kutoka Tunisia na Misri kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi kati ya Taifa Stars na Ivory Coast itakayochezwa Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan.
Mwamuzi atakuwa Slim Jedidi wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Bechir Hassani, wote kutoka Tunisia. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Sherif Hassan kutoka Misri. Mwamuzi wa akiba ni Youssef Essrayri pia kutoka Tunisia.
Mtathmini wa waamuzi (referee assessor) ni Rachid Medjiba kutoka Algeria wakati Kamishna wa pambano hilo atakuwa Saleh Issa Mahamat kutoka Chad. BR>
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). |
added on 2012-05-12 16:44:22 by Admin
Washindi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Simba kesho itakuwa na kibarua cha kujihakikishia inasonga mbele katika mashindano ya kombe la shirikisho la CAF.
Simba SC waliondoka kuelekea Khartoum Sudan tangu jummanne, wakiwa na matokeo mazuri ya mchezo wa kwanza dhidi ya Al-Ahly ulochezwa uwanja wa taifa Dar-es-salaam na Simba kuibuka na na ushindi wa 3-0.
“Tukiwa kama timu pekee ya Afrika Mashariki ilobaki katika mashindano tumefanya maandalizi yakutosha, kwakuwa tunajua Al-Ahly ni timu nzuri pia” alisema Kamwanga.
Wacheza 19 waliosafiri kwaajiri ya mtanange huo wa kesho mei 13,2012 ni Juma Kaseja, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Patrick Mafisango, Uhuru Seleman, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi and Emmanuel Okwi, Ali Mustapha, Obadia Mungusa, Victor Costa, Derrick Walulya, Jonas Gerald, Edward Christopher na Salum Machaku.
Viongozi ni Milovan Cirkovic (kocha mkuu), Amatre Richard (kocha msaidizi), Nico Nyagawa (co-ordinator), James Kisaka (goalkeeper’s coach), Cosmas Kapinga (doctor). |
added on 2012-05-12 16:39:41 by Admin
|
|
|
Rais Yoweri Museveni wa Uganda |
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema hatogombea tena urais wa nchi yake atakapofikisha miaka 75, kama katiba ya Uganda inavyosema.
Akizungumza katika NTV Rais Museveni amesema utafiti wa kisayansi unadhibitisha kuwa mtu anaweza kuwa vizuri akifika miaka 75 ila hatoweza kuongoza kwa ufasaha na umakini.
“nitakapofikisha miaka 75 sitokubaliana na kubadilishwa umri katika katiba ili mimi nipate tena nafasi ya kugombea urais” alisema Rais Museveni.
Kwasasa katiba inamruhusu Mh. Museveni kugombea tena sababu atakuwa chini ya miaka 75 uchaguzi wa 2016 japo akishinda atakuwa na miaka 77 kufikia 2021
|
|